0

Mwamnyeto bado aamini

Mwamnyeto bado aamini

Sat, 8 Aug 2020 Source: Mwanaspoti

BEKI mpya wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema bado aamini kama amemaliza msimu mzima bila ya kuwa majeruhi na kudai hicho ni kitu anachojivunia, kwani hutokea kwa nadra katika soka.

Mwamnyeto amesema kazi yao ina changamoto nyingi ikiwemo majera ambayo wengine wakiumia sana, wanakuwa wanakaa nje kwa muda mrefu bila kufanya kazi, hivyo kwake anaona Mungu amemnusuru.

Amesema anakwenda kwenye timu yake mpya akiwa yupo fiti, hivyo anajisikia mwenye furaha kwenda kuanza maandalizi ya msimu kwa ushindani wa juu, akiwa hana tatizo la aina yoyote mwilini mwake.

"Si jambo jepesi kumaliza msimu bila kuumia kwani kuna kugongana na mchezaji mwenzako, kuna kuanguka wakati wa kazi, lakini yote hayo nimenusurika ndio maana nasema ni jambo kubwa sana kwangu," amesema Mwamnyeto na kuongeza;

"Majeraha ni kitu kibaya kwa mchezaji kwani kazi yetu inategemea miili yetu kuwa fiti, nje na hapo hakuna kinachoweza kufanyika, ndio maana naona kwangu ni muujiza si kwamba nilikuwa makini zaidi kuliko wengine ambao wamekumbwa na hilo."

Mbali na hilo, amefurahia mchezaji mwenzake Ayoub Lyanga kusaini Azam FC kwamba ni hatua nzuri kwake, kuendelea kuonyesha uwezo wake ili kuweza kufika mbali zaidi.

Chanzo: Mwanaspoti

Join our Newsletter