0

Gaucho wa Simba afichua kilichowabeba

Gaucho wa Simba afichua kilichowabeba

Sat, 8 Aug 2020 Source: Mwanaspoti

NAHODHA wa timu ya soka ya Wanawake ya Simba Queens, Mwanahamis Omary 'Gaucho' amesema kufanya kwao vizuri katika Ligi Kuu ya Wanawake, kumetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata kutoka kwa viongozi wao.

Simba Queens ilitangazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo katika mchezo uliopita dhidi ya Baobab Queens baada ya kuwabugiza mabao 5-0 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Gaucho, hiyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio yao, kama ambavyo walihaidi kabla ya ligi kuanza huku pia ushirikiano na umoja wa wachezaji pia nao umechagiza mafanikio hayo.

"Tunamshukuru sana Mungu, maana yeye ndiye kila kitu kwetu, tumetwaa ubingwa huu ni furaha kubwa kutimiza malengo ambayo tulijiwekea kabla hata ya ligi kuanza," amesema nyota huyo na kuongeza;

"JKT Queens walikuwa mabingwa watetezi ni moja ya timu yenye ushindani mkubwa lakini tuliwaambia watuache tu msimu huu hatutaki utani."

Naye kocha wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi aliwapongeza wachezaji wake kwa nidhamu ya hali ya juu ambayo waliionyesha toka mwanzo hadi mwisho.

Chanzo: Mwanaspoti

Join our Newsletter