0

Biashara, JKT zatakata Ligi Kuu

Biashara, JKT zatakata Ligi Kuu

Mon, 22 Feb 2021 Source: HabariLeo

BIASHARA United na JKT Tanzania zimewafurahisha mashabiki wao baada ya kuchomoza na pointi tatu kila moja kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa jana.

Katika mchezo uliochezwa mchana, Biashara United iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Karume, Musoma, mkoani Mara.

Katika mchezo huo ambao Biashara walitawala walijihakikishia ushindi huo kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Christian Zinga dakika ya 36, Lenny Kisu dakika 45 na la tatu likipachikwa wavuni na Yusuph Athuman dakika ya 68.

Katika mchezo uliochezwa jioni, JKT Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coasta Union, mchezo uliokuwa na ushindani mkali ukichezwa Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Mabao ya wenyeji JKT Tanzania yaliwekwa kimiani na Rashid Mandawa dakika ya 47 na la pilli likifungwa na Daniel Lyanga dakika 66.

Kwa matokeo hayo, Bishara United Imefikisha pointi 35 na Inaendelea kukalia nafasi ya nne, huku JKT Tanzania ikishika nafasi ya 10 kwenye msimamo ikiwa na pointi 24.

Ruvu Shooting inabaki katika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 31, huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 13 na pointi 23 walizokusanya kwenye michezo 21 waliyokwisha cheza.

Chanzo: HabariLeo