0
MenuInfos
Dini

Dodoma Jiji FC yaacha wachezaji 12

Sat, 8 Aug 2020 Source: habarileo.co.tz

TIMU ya Dodoma Jiji FC imeanza kujiimarisha kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara baada ya kusajili wachezaji watatu na kuacha 12.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo ya Habari na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ramadhan Juma, wachezaji wapya waliowasajili ni Cleophance Mkandala kutoka Tanzania Prisons, Michael Chinedu wa Alliance na Seif Karihe wa Lipuli.

Wachezaji hao wote wamesajiliwa wakiwa wamemaliza mikataba yao huko walikotoka, ambapo Alliance na Lipuli zimeshuka daraja.

“Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Agosti 1, mwaka huu timu imeendesha zoezi la usajili kwa mujibu wa mapendekezo ya benchi la ufundi,”ilisema taarifa hiyo.

Wachezaji walioachwa ni Yusuf Abdul, Joseph Mapembe, Hamad Kibopile, Rajabu Kibera, Joshua Soka, Aziz Gillah, Shaban Mocka, James Mendy, Ismail Makorosa, Moshi Mrisho, Mohamed Kilua na Ramadhan Mohamed ambaye amerejeshwa Azam FC baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika.

Aidha, ilitaja walioongezewa mikataba kuwa ni Emmanuel Mseja, Hussein Masangala, Anderson Solomoni, Hassan Kapona, Mbwana Kibacha, Rajabu Seif, Steven Mganga, Jamal Mtegeta, Deusdelius Kigawa, Santos Thomas na Khamis Mcha.

Timu hiyo ni miongoni mwa tatu zilizopanda msimu huu baada ya kufanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza. Nyingine zilizopanda ni Gwambina ya Mwanza na Ihefu ya Mbeya.

Chanzo: habarileo.co.tz

Join our Newsletter