0

Youth shade foundation walivyoadhimisha siku ushairi wa watoto

Youth shade foundation walivyoadhimisha siku ushairi wa watoto

Tue, 6 Oct 2020 Source: Millard Ayo

Taasisi ya Youth Shade Foundation imefanya tamasha la Siku ya Ushairi wa Watoto Duniani (WoChiPoDa au World Children’s Poetry Day), adhimisho hilo lilifanyika katika kituo cha watoto yatima cha tuleeni kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Vijijini.

Siku hii huadhimishwa kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi October kila mwaka, WoChiPoDa ilianzishwa mwaka 2014 na mzaliwa wa Tanzania Gloria D. Gonsalves anayeishi Ujerumani.

Gloria ni mtunzi wa hadithi za watoto na mashairi, lengo la mradi huu ni kujenga mapenzi ya ushairi na kuelimisha watoto sanaa ya ushairi katika mandhari nje ya shule.

Taasisi ya Youth Shade Foundation ikiongozwa na Brian Mlingi pamoja na walezi wa Kituo cha Tuleeni waliwaandaa watoto kujumuika na kushiriki siku hii katika uimbaji wa mashairi na kuwapa mafundisho juu maisha yao. Baada ya hayo watoto walishiriki chakula kwa pamoja na michezo mbalimbali.

Youth Shade Foundation ni shirika lisilo la kiserekali linalohusika na kusaidia vijana na watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu ama hatarishi Pamoja na watoto yatima pia ni mawakala wa utunzaji wa Mazingira.

Chanzo: Millard Ayo