0

Wema atoa ya moyoni

Wema atoa ya moyoni

Sat, 3 Oct 2020 Source: HabariLeo

MWIGIZAJI na aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ameendelea kuchukizwa na baadhi ya mastaa wa fi lamu ambao wamekuwa wakimbeza na kumkejeli kutokana na kujikondesha kwake.

Wema aliyasema hayo baada ya mwigizaji wa filamu na mchekeshaji mwenzake, kuandika maneno ambayo alihisi kumlenga yeye, hivyo akaamua kumjibu kupitia mtandao huo wa kijamii kwamba si kila kitu ni utani.

Aliongeza kwa kusema kwamba hajapenda utani ambao amekuwa akifanyiwa kwa kuwa kila kitu si utani na kama angekuwa na mamlaka yoyote angeweza kumuweka ndani msanii huyo.

“Sijapenda na si kila kitu ni utani, ningekuwa na mamlaka ningekuweka ndani,” alisema. Mwigizaji huyo amekuwa akiingia kwenye changamoto ya kuongelewa vibaya tangu alipoamua kujikondesha.

Chanzo: HabariLeo