0

Wema, Jaydee, wang’ara Nigeria

Wema, Jaydee, wang’ara Nigeria

Fri, 23 Oct 2020 Source: HabariLeo

WASANII watatu wa Tanzanaia wamepata tuzo za Hapa zilizofanyika Nigeria Jumapili iliyopita.

Katika tuzo hizo za nne ambazo mshereheshaji alikuwa Zarina Hassan wasanii walioshinda ni Judith Wambura ‘Lady- Jaydee’, Christian Bella na Wema Sepetu.

Lady Jaydee alishinda katika kipengele cha mwanamuziki bora wa kike wa Afrika wa Afrobeat, Bella alishinda katika kipengele cha msanii bora wa kujitegemea wa Afrika na Wema kipengele cha mwigizaji bora wa TV series kwa Afrika na Hollywood.

Baada ya kutangazwa mshindi Lady Jaydee aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akishukuru tuzo za Hapa kwa kumchagua.

“Asante Hapa awards kwa kunichagua,” aliandika.

Tuzo za Hapa ni muunganiko wa jina la Hollywood na Afrika (HAPAwards) ni tuzo zinazohusisha waigizaji, wanamuziki na wachekeshaji wenye mafaniki

Chanzo: HabariLeo