0

Wajanja waliojimilikisha pisi kali za Kenya

Wajanja waliojimilikisha pisi kali za Kenya

Fri, 30 Oct 2020 Source: Mwanaspoti

By KELVIN KAGAMBO LINAPOKUJA suala la mahaba, mastaa wengi wa kiume wa Bongo wanaonekana kunasa kwa urahisi kwenye ulimbo wa mademu kutoka nchi jirani. Harmonize ana demu wa Kitaliano, Jux alikwenda China kusoma akahitimu na demu wa Kifilipino, Linex alikuwa na pisi ya kizungu kutoka Finland na listi inaendelea. Jamaa hawana mchezo.

Lakini, licha ya kuwa pisi kali za nje zinawindwa sana na wasanii wa Bongo, inaonekana ni kama vile windo jepesi zaidi kwa mabraza ni hapo nchi jirani ya Kenya. Na ili kuthibitisha hilo, hii hapa listi ya mastaa wa kiume kutoka Bongo waliowahi kuthibitika kuwa na mabebi kutoka Kenya.

A.Y

Kabla ya kufunga ndoa na mkewe kutoka Rwanda anayeitwa Remy, mzee wa komesho aliwahi kunasa kwa msanii kutoka Kenya, Cecilia Wairimu maarufu Amani. Na za chinichini zinasema ilibaki kidogo tu wawili hawa wawe mke na mume kabla ya jini mkata-kamba kuingia kati na kuvuruga mipango.

AY na Amani walikutana mwaka 2005 huko huko Kenya, ambapo kwanza walikuwa marafiki kisha wapenzi kabla ya 2007 kupigana kibuti, huku sababu ikitajwa kuwa ni umbali na gharama za kuhakikisha penzi hilo linafanya kazi.

“Mimi sikuwa tayari kuhamia Kenya, naye hakuwa tayari kunifuata Tanzania. Kwa hiyo umbali ulifanya tushindwe kuwa pamoja.” alieleza A.Y kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari.

Chanzo: Mwanaspoti