0

Tamasha la muziki la Marafiki kukutanisha wadau wa Muziki

Tamasha la muziki la Marafiki kukutanisha wadau wa Muziki

Wed, 7 Oct 2020 Source: Mwanaspoti

By SALOME GREGORYVIKUNDI 13 vya wanamuziki wa Tanzania na mmoja wa Kenya vitatumbuiza kwenye tamasha la kwanza la muziki liitwalo Marafiki litakalofanyika kwa siku tatu sehemu mbili tofauti ikiwemo Dar es Salaam na Bagamoyo.

 

Mkurugenzi wa Tamasha hilo Isack Abeneko amesema tamasha hilo litafanyika kuanzaio keshokutwa Alhamisi, Oktoba 8 hadi 10 mwaka huu.

 

Tamasha hilo lenye kauli mbiu Utamaduni ni ngao ya Taifa litafanyika Slow Leopord Masaki Oktoba 8 na 9 na Oktoba 10 tamasha litakua Bagamoyo Firefly kwa kiingilio  cha Sh10,000 ambapo tamasha litaanza saa 1 jioni mpaka saa sita usiku kila siku.

 

Chanzo: Mwanaspoti