0

"Sisi tumekuwa wakali kutokana na aina ya wagombea"Katibu kamati ya Maadili

Tue, 27 Oct 2020 Source: millardayo.com

“Sisi tumekuwa wakali kutokana na aina ya wagombea tulionao kwa sasa, ndiyo wamesababisha watu waone mbona adhabu zimekuwa nyingi na kamati imekuwa kali hivi” Katibu wa Kamati ya Maadili ya Taifa, Emmanuel Kawishe

“Vyama vya siasa ni vile vile, adhabu ni zile zile tofauti ni wagombea, unakuta Mgombea anakiuka maadili halafu anakimbilia kwenye vyombo vya habari” Katibu wa Kamati ya Maadili ya Taifa, Emmanuel Kawishe

“Mtu kulalamika siyo lazima awe ametendewa vibaya, inawezekana kile alichotaka yeye hakijafanyika hivyo akalalamika na kuna mwingine kulalamika ni asili yake hata umfanyie nini” Katibu wa Kamati ya Maadili ya Taifa, Emmanuel Kawishe

“Dira yetu sisi inalenga kuratibu na kuendesha chaguzi ambazo zinazingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria za uchaguzi na uchaguzi ambao ni shirikishi, uchaguzi wa uwazi zaidi” Katibu wa Kamati ya Maadili ya Taifa, Emmanuel Kawishe

BODABODA WAKUTANISHWA KAGERA, “TUKAPIGE KURA, TUILINDE AMANI YETU”

Chanzo: millardayo.com