0

Serikali yaanzisha mfuko wa wasanii

26b6587e3312013e0f5e60a2109e9765 Serikali yaanzisha mfuko wa wasanii

Sat, 14 Nov 2020 Source: habarileo.co.tz

SERIKALI imeanzisha mfumo rasmi utakaowawezesha wasanii kudai na kupata haki zao stahiki kwa wakati.

Kauli hiyo ilitolewa kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma jana na msemaji wa serikali na Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas baada ya kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa bunge la 12 iliyotolewa na Rais John Magufuli.

Alisema atajitahidi kutafsiri hotuba ya Rais Magufuli kwa umakini na kuifanyia kazi ikiwemo kusimamia haki za wasanii kwa kuhakikisha wanatengeneza kazi bora.

“Rais tangu anaapishwa na leo (jana) nimesikia akizungumzia zaidi sekta ya sanaa kwa kuhakikisha tunawakuwa na wasanii ambao haki zao wanazipata,” alisema Abbas.

Alisema tayari mifumo wameshaianzisha kuhakikisha wasanii wanapata haki zao kirahisi kwa kuanzisha mfuko ikiwemo Cosota kuhamishwa kwenda kwenye ofisi yake.

“Kubwa zaidi leo (jana) Rais ameongelea zaidi kuanzishwa kwa mfumo wa sanaa na utamaduni mfumo ambao wadau wataenda kuomba mikopo na kupata elimu umeshaanzishwa kinachosubiriwa ni utekelezaji tu,”alisema Abbas.

Alisema mipango waliyonayo ni kuboresha mifumo kwa kuwasaidia wasanii kupitia kazi zao kuuza kwa tehama na kupata faida yao inayotakiwa.

Chanzo: habarileo.co.tz