0

Nandy ala shavu la maana TTCL

Initiative Ed 0 Nandy ala shavu la maana TTCL

Thu, 10 Jun 2021 Source: ippmedia.com

Hafla ya makubaliano hayo ilifanyika Ofisi za TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam ambako uongozi wa EASTWAVE MARKETING ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha hilo waliomba TTCL kushirikiana nao katika kufanikisha tukio hilo nchini na Afrika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Biashara kutoka TTCL, Vedastus Mwita, alisema kuwa baada ya mchakato wa kibiashara kukamilika, TTCL imekuwa mdhamini mkuu wa tamasha hilo ambalo kuanzia sasa litaitwa 'TTCL Nandy Festival 2021- Watakaa Tu'.

Tamasha hili litafanyika katika mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Rukwa, Kigoma, Shinyanga, Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Zanzibar huku matarajio yakiwa ni wananchi wa mikoa hiyo na visiwa vya Zanzibar kupata burudani ya muziki yenye ubora na kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wa Nandy, alisema TTCL kujitoa na kuwa mdhamini mkuu si jambo dogo, akilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kutumia tamasha lake kuwarudisha Watanzania nyumbani kupitia burudani atakayoitoa katika mikoa iliyoandaliwa.

Chanzo: ippmedia.com