0

Nandy, Ali Kiba wafanya mambo

Nandy, Ali Kiba wafanya mambo

Sun, 15 Nov 2020 Source: HabariLeo

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ametimiza ndoto zake za kufanya wimbo wa ushirikiano na mkongwe Ali Kiba baada ya kuachia ngoma mpya wa Nibakishie.

Huko nyuma msanii huyo aliwahi kusema moja ya watu anaotamani kufanya nao kazi ni msanii huyo anakubali kazi zake.

Kupitia mtandao wake wa kijamii aliweka picha akiwa na Ali Kiba kuwahabarisha mashabiki wake wimbo mpya waliofanya pamoja.

Kutoa wimbo huo hakika ni mafanikio makubwa kwake msimu huu wa 2020 kwani anaweza kuwa ndiye msanii wa kike anayezidi kufanya vizuri kwa nyimbo za ushirikiano.

Ndani ya mwaka huu ametoa nyimbo kadhaa zikiwemo Na Nusu, Acha Lizame akiwa amemshirikisha Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Dozi, Do Me akiwa amemshirikisha Billnas na zote zimefanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali.

Chanzo: HabariLeo