0

"Na mimi nifunguliwe, kazi inaendelea Mama" Gigy amlilia Rais Samia

"Na mimi nifunguliwe, kazi inaendelea Mama" Gigy amlilia Rais Samia

Tue, 6 Apr 2021 Source: Millard Ayo

Msanii wa BongoFleva Gigy Money ameomba kufunguliwa adhabu yake ya miezi 6 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kusema Vyombo vya Habari vilivyofungwa vifunguliwe ila wafuate sheria na miongozo ya Serikali.

“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, sijui viji- TV vya mikononi vile ‘online’, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe” Rais Samia Suluhu Hassan 

Baada ya Samia Suluhu Hassan kusema hivyo msanii Gigy Money amecomment’ kwenye post iliyopost kwenye Millard Ayo “Na mimi nifunguliwe jamani, kazi inaendelea mama“.

Chanzo: Millard Ayo