0

Mzee Yusuf aibuka kivingine

Mzee Yusuf aibuka kivingine

Sat, 8 Aug 2020 Source: HabariLeo

BAADA ya kukaa kimya kwa muda wa mika mitano, mfalme wa muziki wa miondoko ya taarabu, Mzee Yusuf amesema anarejea tena kwenye tasnia hiyo kwa kutambulisha mfumo mpya wa kuimba ili kuendelea kuwavutia mashabiki.

Mfumo huo alitarajia kuutambulisha jana kwenye tamasha lake la kwanza kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo maeneo ya Mbagala Temeke tangu kutanganza kurejea tena kwenye muziki huo.

Akizungumza Dar es Salaam, Yusuf alisema mpango wake ni kuuboresha muziki huo ili soko lake lipanuke kimataifa lakini baada ya kukaa nje kwa muda, amegundua upungufu ambao amepanga kuanza kuufanyia kazi.

“Narudi kwenye muziki wa taarabu kwa kuwaondoa mashabiki sehemu walipo na kufanya mapinduzi makubwa kwa kuja na mfumo mpya ambao watu walikuwa hawajauzoea, kwanza kuwafanya kuanza kutumia mtandao wa youtube kuangalia matukio na pili kuwaonesha stahili ya kupiga muziki, ”alisema Yusuf.

Alisema kwa muda mrefu mashabiki wa muziki wa taarabu walizoea kuangalia matukio kwenye simu zao lakini kwa sasa anakuja na mfumo wa kuwazoesha kujua umuhimu wa mitandao.

Yusuf alisema duniani kote muziki unapigwa vilevile lakini msanii ana uwezo wa kufanya maboresho ya aina ya uchezaji na kuwahamisha mashabiki kuanza kupenda mfumo mpya ambao na utambulisha leo (jana).

Aidha, amewaomba mashabiki wa muziki huo kumpokea kwa moyo mmoja kama ilivyokuwa huko nyuma na kuahaidi kuendelea kuachia vibao vipya ili kuendelea kuwapa burudani kama zamani.

Chanzo: HabariLeo

Join our Newsletter