0

Mwana FA ashinda Ubunge Muheza

Mwana FA ashinda Ubunge Muheza

Fri, 30 Oct 2020 Source: Millard Ayo

Msanii Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amefanikiwa kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Muheza,Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’ akimshinda mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.

Mwana Fa anaungana na wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule ‘Prof Jay’ aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.

HOTUBA NZITO YA MWINYI BAADA KUSHINDA URAIS ZANZIBAR “”Mimi Hussein Mwinyi si bora”

Chanzo: Millard Ayo