0

Mbunge wa mteule wa CHADEMA asema hatawasaliti wananchi waliomchagua

Mbunge wa mteule wa CHADEMA asema hatawasaliti wananchi waliomchagua

Tue, 3 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Aida Khenan, Mbunge Mteule wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA amesema, hatowasaliti wananchi waliomchagua hivyo atakwenda Bunge kuapishwa ili aweze kuwatumikia.

Aida ni Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CHADEMA aliyetangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, akimshinda Ally Kessy wa CCM aliyekuwa anatetea jimbo hilo aliloongoza kwa miaka 10.

Kauli hiyo imekuja baada CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kutoyatambua matokeo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hata kwenye maeneo waliyoshinda.

Katika Bunge lililopita, Aida alikuwa Mbunge wa Viti Maalum. Lakini sasa amesema yeye ni Mbunge ambaye anasubiri kuapishwa.

BAADA YA UCHAGUZI WAFANYABIASHARA KARIAKOO WATOA TAMKO “TUFANYE KAZI TULIPE KODI”

Chanzo: Millard Ayo