0

Majaliwa amjulia hali King Kiki "anaumwa mgongo" (+video)

Video Archive
Sun, 8 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa leo amemtembelea na kumjulia hali mwanamziki mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii, Nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ally, Jijini Dar es Salaam.

Majaliwa amempa pole Kikii anayesumbuliwa na matatizo ya Mgongo na amemtakia pona ya haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

King Kiki ni mmoja wanamuziki wakongwe nchini Tanzania na amewahi kuvuma kwa nyimbo kadhaa miongoni mwake ikiwa “Kitambaa cheupe”.

Chanzo: Millard Ayo