0

"Magaidi 300 walivamia Mtwara" IGP Sirro (+video)

"Magaidi 300 walivamia Mtwara" IGP Sirro (+video)

Thu, 22 Oct 2020 Source: Millard Ayo

“Ni kweli Wiki iliyopita, Magaidi wapatao 300 walitoka Msumbiji walivamia kituo chetu pale Kijiji chetu cha Kitaya (Mtwara), walifanya uhalifu mbalimbali na walifanya mauaji, tumefuatilia na baadhi ya Watuhumiwa kadhaa siwezi kuwataja wamekamatwa kuhusika na hayo matukio ambao wengine ni wa kwetu hapa walishirikiana na wengine kutoka nje”– IGP Sirro“Kwakuwa tunaendelea na huo mtandao siwezi kusema sana lakini niwahakikishie Watanzania kwamba siku zote huwa nasema damu ya Mtanzania haipotei bure, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji waliobaki tumewakamata tunaendelea kuwahoji kuhusu mtandao mzima”– SIRRO

“Watanzania waelewe huu ni mtandao ambao ulianzia Rufiji, Kibiti wengine tulipambana nao wakaona wameshindwa wakakimbilia Msumbiji, kule wameungana na wenzao wanajaribu kurudi nyumbani, tumejipanga kuwa wakirudi tutawashughulikia na hata wakibaki huko tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha hawatokuwa salama”– SIRRO

View this post on Instagram

"Ni kweli Wiki iliyopita, Magaidi wapatao 300 walitoka Msumbiji walivamia kituo chetu pale Kijiji chetu cha Kitaya (Mtwara), walifanya uhalifu mbalimbali na walifanya mauaji, tumefuatilia na baadhi ya Watuhumiwa kadhaa siwezi kuwataja wamekamatwa kuhusika na hayo matukio ambao wengine ni wa kwetu hapa walishirikiana na wengine kutoka nje"- IGP Sirro "Kwakuwa tunaendelea na huo mtandao siwezi kusema sana lakini niwahakikishie Watanzania kwamba siku zote huwa nasema damu ya Mtanzania haipotei bure, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji waliobaki tumewakamata tunaendelea kuwahoji kuhusu mtandao mzima"- SIRRO "Watanzania waelewe huu ni mtandao ambao ulianzia Rufiji, Kibiti wengine tulipambana nao wakaona wameshindwa wakakimbilia Msumbiji, kule wameungana na wenzao wanajaribu kurudi nyumbani, tumejipanga kuwa wakirudi tutawashughulikia na hata wakibaki huko tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha hawatokuwa salama"- SIRRO #MillardAyoUPDATES (

Chanzo: Millard Ayo