0

MWANAMZIKI NGULI AVUNJIKA MGUU AKIWA USINGIZINI

MWANAMZIKI NGULI AVUNJIKA MGUU AKIWA USINGIZINI

Thu, 12 Nov 2020 Source: Zanzibar 24

Mwanamziki mkongwe wa bendi ya Talent nchini Tanzania, Hussein Jumbe katika hali isiyo ya kawaida amepata ajali akiwa amelala (ndotoni) na kuvunja Mguu wake wa Kulia .

Mzee Jumbe ambae aliwahi kutamba na wimbo wake wa “Nachechemea” uliojizolea umaarufu Mkubwa sana, anasema kuwa hadhani kuwa ndoto hiyo ni ya kawaida Ila yote anamuachia Mungu .

Msanii huyo alisema kuwa aliota anakimbizwa na kuku na kujikuta akimpiga mateke, kumbe alikua anapiga Ukuta kitu kilichompelekea kuvunja Mguu wake wa kulia .

Chanzo: Zanzibar 24