0

MKOJANI-3: Huyo Tin White mbona freshi tu!

MKOJANI-3: Huyo Tin White mbona freshi tu!

Sat, 20 Feb 2021 Source: Mwanaspoti

By Kelvin KagamboMore by this AuthorBy Olipa AssaMore by this Author KATIKA toleo lililopita Mkojani alielezea maisha yake kwa undani tangu kuwa staa. Alielezea mambo ya maendeleo aliyoyafanya, pia aliweka wazi kuhusu namna watu wanavyomchukilia na yeye alivyo.

Katika toleo hili anaongelea mambo muhimu kuhusu sanaa yake ikiwemo tetesi za kuwepo kwa ugomvi kati yake na wachekeshaji wenzake Tin White na Ringo. Shuka nayo

UGOMVI NA TIN WHITE

Kwa namna moja ama nyingine unaweza kusema wachekeshaji Tin White na Ringo ndiyo waliompa umaarufu Mkojani wakati alipoanza kuigiza kwa jina la Kipupwe.

Kipindi hiko alikuwa akiigiza kwenye filamu za swahiba zake hao ambao walikuwa maarufu zaidi yake, na hata alipoanza kupata umaarufu bado alienda kuigiza nao bega kwa bega.

Chanzo: Mwanaspoti