0

Lina amtambulisha mchumba wake

Lina amtambulisha mchumba wake

Wed, 4 Nov 2020 Source: HabariLeo

NYOTA wa kike wa muziki wa kizazi kipya, Lina Sanga ‘Linah’ amemtambulisha mchumba wake ili kufuta mitazamo ya watu kuwa hajatulia.

Linah alisema ameamua kumuonesha mchumba wake kwa sababu wanapendana na wana malengo.

“Mtu wangu sio maarufu ila alitaka nimtambulishe kwa watu wajue kuwa nina mtu ndio maana nikefanya hivyo," alisema alipohojiwa na East Afrika Televisheni.

Alisema yeye sio mjinga kufanya kitendo hicho na kwamba imepita miaka minne bila ya kumweka mwanaume yeyote mtandaoni baada ya kuachana na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja.

Msanii huyo alisema hata kama ikitokea wameachana hatajutia kwani atapata mwingine.

Kabla ya kumweka mwanaume huyo mpya katika mtandao wake wa Instagram hivi karibuni, alikuwa akihusishwa kwenye mahusiano na wanaume tofauti kitendo ambacho alisema kilimfanya mpenzi wake huyo kumhofia.

Chanzo: HabariLeo