0

Kamikaze na walinzi 10 wa kimasai

Kamikaze na walinzi 10 wa kimasai

Sun, 15 Nov 2020 Source: HabariLeo

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Cyril Kamikaze anatembea na walinzi 10 wa kimasai kwa ajili ya kulinda usalama wake.

Akizungumza Dar es Salaam kuhusu ulinzi huo, Kamikaze alisema kuwa na walinzi haimaniishi kuwa na maadui wengi isipokuwa yeye kama msanii mkubwa na maarufu ni muhimu kwa usalama wake.

“Mimi ni msanii ninayetaka kutoka tofauti, hawa jamaa nina ukaribu nao kwa muda mrefu ninafanya nao kazi, niko salama sana nikiwa nao,”alisema wakati akihojiwa na Bongo 5.

“Ulinzi ni kitu muhimu hasa kwetu wasanii kuna muda mashabiki wanaweza kukuvamia kwa nia njema mtu anaweza kufurahi ameshika chupa yake ya bia akaja kukukumbatia akakugonga bahati mbaya,”alisema.

Msanii huyo ambaye amepotea kwa zaidi ya mwaka alisema kwa sasa amekuwa akikabiliwa na majukumu ya kibiashara na shughuli nyingine binafsi ila muda sio mrefu atarejea kimuziki, kwani kuna miradi mingi inakuja mbele.

Chanzo: HabariLeo