0

Harmonize, Nandy, Jux uso kwa uso kwenye album mpya ya Abbah

Thu, 25 Feb 2021 Source: millardayo.com

NI Headlines za mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Abbah ambae time hii anatarajia kuzindua rasmi album yake aliyoipa kwa jina la The Evolution ambayo amewakutanisha wasanii kutoka sehemu tofauti za bara la Afrika.

Album hilo inatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Mwanza FEB 27TH mahali ni Malaika Bech Resort Elevate ambapo mashabiki ama wadau wa muziki wataweza kushuhudia live burudani uzinduzi wa album hiyo huku burudani ikitolewa na wasanii akiwemo Juma Jux, Darassa, Mario Mota The Future.

Tazama Tracklist zinazopatikana katika album hiyo mpya ya Abbah ‘The Evolution’

Chanzo: millardayo.com