0

Hamisa: Sipendi mtoto wangu kulinganishwa

Fri, 16 Oct 2020 Source: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI, Hamisa Mobetto, amesema hapendi mtu amlinganishe mtoto wake na watoto wengine.

Hamisa alieleza hisia zake kwenye kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, Dar es Salaam juzi,ambapo pia alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu yeye na kazi zake.

"Kitu ambacho sikipendi ni mtu kujaribu kumlinganisha mtoto wangu na watoto wengine, kiukwe sipendi," alisema.

Pia alisema kabla ya kumzaa Dylan alibeba ujauzito wa Diamond Platnumz mara tatu lakini ukaharibika bahati mbaya.

“Kabla sijapata mimba ya Dylan nilipata ujauzito wa Diamondi mara tatu na bahati mbaya zikaharibika,” alisema.

Katika hatua nyingine,Hamisa alisema ana mpango wakufanya kolabo ya wimbo na Tanasha kutoka nchini Kenya.

“Mimi na Tanasha tumezungumza na tayari tuna mpango wakufanya kolabo hivi karibuni,” alisema.

Hamisa na Tanasha wote ni wazazi wenza wa Diamond Platnumz.

Chanzo: habarileo.co.tz