0

Esma, Msizwa hakuna ndoa

Esma, Msizwa hakuna ndoa

Thu, 5 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By NASRA ABDALLAHIKIWA imepita miezi mitano tangu afunge ndoa na mfanyabiashara, Msizwa, ndoa hiyo inaonekana haipo tena

Esma na Msizwa walifunga ndoa Juni mwaka huu 2020.

Katika ndo hiyo, Esma ambaye ni dada huyo wa msanii mkubwa nchini Tanzania, Diamond Platnumz alikuwa anaolewa mke wa tatu katika familia ya mfanyabiashara huyo.

Ni kwa muda sasa huko mitandaoni Esma ameonekana kuwa kimya jambo ambalo watu hawajalizoea, kwani tangu kufungwa kwa ndoa hiyo kila wakati alikuwa akiweka mapichapicha akiwa maeneo tofauti na mume wake huyo.

Ukimya huo ulifanya watu kujiuliza maswali mengi na wengine kwenda mbali kuwa huenda wawili hao wameachana.

Maswali hayo yamejibiwa jana na Esma mwenyewe, wakati alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram, ambapo alitoa nafasi ya watu kumuuliza swali lolote.

Chanzo: Mwanaspoti