0

Ebitoke aingia katika muziki

Ebitoke aingia katika muziki

Sun, 15 Nov 2020 Source: HabariLeo

NYOTA mchekeshaji nchini Anastasia Exavery ‘Ebitoke’ amesema ameamua kuthubutu kuingia katika fani nyingine ya muziki kwa kuwa anapenda.

Akizungumza Dar es Salaam, msanii huyo alisema ameona anaweza kufanya muziki ndio maana amejiingiza huko na sasa ameachia ngoma yake mpya inayoitwa Solo.

“Nimeona ninaweza kufanya muziki nimethubutu, hata kuimba kwenyewe kwa lugha ya kiingereza, nimeona niingie kote kwenye uchekeshaji na kuimba naweza kufanya yote,”alisema wakati akihojiwa na East Afrika Televisheni.

Msanii huyo alisema anajivunia mafanikio katika sanaa anayofanya, kwani maisha anayoishi leo sio kama yale ya zamani, kuna mambo mengi anajivunia yamebadilika.

Alisema kwa sasa ana kiwanja na anatamani kuwa na nyumba yake, lakini kingine amepanga na anaishi na mama yake mzazi pamoja na mdogo wake.

Ebitoke alisema maisha aliyokuwa akiishi miaka iliyopita yalikuwa sio halisi alikuwa anaigiza na kufanya kiki ila sasa ni mtu anayejitambua.

Chanzo: HabariLeo