0

Diamond kicheko kuonana na wanae

Diamond kicheko kuonana na wanae

Fri, 6 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By NASRA ABDALLAHJANA Alhamis Novemba 5, 2020 itakuwa siku ya historia kwa msanii wa Tanzania Diamond, Platnumz, baada ya kukutana na watoto wake, ambao hakuonana nao kwa miaka miwili.

Watoto hao ni Nillan na Latifa ambao alizaa na mjasirimali kutoka Uganda, Zarina Hassan maarufu Zari.

Zari na Diamond kwa muda wa miaka miwili hawakuwa katika mahusiano mazuri ambayo pia yaliathiri ukaribu wa watoto na baba yao.

Wawili hao mahusiano yao yalikufa tangu Februari mwaka 2018, na hii ni baada ya Zari kutangaza jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwamba msanii huyo amekuwa akimsaliti kwa kuwa na wanawake wengine.

Hata hivyo mawasiliano ya wawili hawa yalionekana kurejea Aprili, 2020 na hii ni baada ya Zari kumnanga Diamond kwa hatua yake ya kutangaza kuzilipia familia 500 kodi ambapo mama huyo wa watoto watano, alisema msanii huyo anafnya hivyo kwa watu huku akiwa hajui watoto wake Afrika Kusini wanakula nini.

Unaweza kusema kampeni hiyo ndio ilirejesha amani kati yao, kwani Diamond alipohojiwa na moja ya vituo vya televisheni nchini alikiri ujumbe huo wa mama watoto wake kumuumiza kiasi cha kutaka kumjibu vibaya lakini uongozi wake ulimsihi asifanye hivyo.

Chanzo: Mwanaspoti