0

DNA ya nini? Mastaa wanaofanana na watoto zao ile mbaya

DNA ya nini? Mastaa wanaofanana na watoto zao ile mbaya

Sun, 18 Oct 2020 Source: Mwanaspoti

Wakati Hamisa Mobetto anatambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha Singh wa Nigeria, mtangazaji wa redio aliyokuwa anatambulisha wimbo huo alimuuliza kuhusu tetesi za kwamba mzazi mwenzake, Diamond Platnumz aliwahi kuwa na wasiwasi kwamba yeye sio baba halisi wa mtoto wao, Dylan hivyo ilibidi waende wakapime DNA — Hamisa akathibitisha kwamba jambo hilo ni kweli.

Akaongeza kwamba: “Tulienda hospitali, tukapima na baada ya wiki kama mbili tatu hivi majibu yakaja na mtoto akaonakena ni wake kwa asimili zote.”

Kwa kawaida wanaume wengi huwa na wasiwasi kuhusu ukweli wa nani baba wa mtoto pale tu inapotokea kuwa mtoto hafanani na mzazi huyo wa kiume. Sasa wakati upande mmoja wa shilingi kuna mastaa wana wasiwasi na watoto wao mpaka kufikia hatua ya kuhitaji DNA (sio kitu kibaya kupima DNA), upande mwingine kuna wasanii ambao wenyewe wana amani kwa sababu kwao walipiga ‘fotokopi’. Yaani watoto waliopata wanafanana nao mpaka unajiuliza DNA ya nini? Listi ya wasanii hao hii hapa.

Mwana-FA

MwanaFA ana watoto wawili wa kike, wa kwanza anaitwa Maleeka na mzuwanda wake mwenye miaka miwili. Ukiwaona watoto hao hasa huyo wa pili wala huhitaji kupewa mchambuzi akusaidie kuelewa kuwa ni mtoto wa damu ya Mwanafalsafa.

Kuanzia rangi nyeupe ya ngozi, midomo yenye rangi ya pinki, mpangilio wa meno kinywani mpaka mwanya - yaani watoto wamechukua kila kitu kama kilivyo kutoka kwa dingi yao. Septemba, mwaka jana, MwanaFA aliposti picha Instagram akiwa na watoto wake kwenye gari, kilichotokea baada ya hapo ilikuwa ni mfululizo wa comment za masihara kutoka kwa mastaa wenzake wakiomba mbinu aliyoitumia kupata watoto anaofanana nao kiasi hicho, kwa mfano Elizabeth Micheal ‘Lulu’ aliandika: “Nyinyi ni mapacha watatu.”

Chanzo: Mwanaspoti