0

Clouds TV yazindua tamthilia yake ya kwanza 2021

Clouds TV yazindua tamthilia yake ya kwanza 2021

Mon, 22 Feb 2021 Source: Millard Ayo

Siku ya leo Clouds TV imezindua tamthilia yake ya kwanza kwa 2021 ambayo itakuwa ikirushwa siku ya Alhamis na kurudiwa siku ya Ijumaa na Jumamosi kupitia Clouds TV.

Program Meneja wa Clouds TV Dotto Bahemu amesema….>>>”Kama ilivyokawaida ya Clouds TV tangu ilipoanzishwa ni kukuza na kuendeleza Sanaa yetu, Leo Clouds TV tunaitambulisha tamthilia mpya inayoitwa Bouteille vide, (chupa tupu) itakuwa inaruka mara moja kwa wiki na itaanza Alhamis hii ya February 25,2021

Muda ni SAA 12 na nusu jioni mpaka saa 1 kamili usiku, na marudio yatakuwa ni Ijumaa kuanzia SAA 5 na 15 na Huu ni mwanzo tu sisi tumeona tushirikiane Na watayarishaji wetu wa ndani kukata Kiu ya waTanzania walio wengi”

Tamthilia hiyo ambayo imepewa jina la Bouteille Vide ambalo ni neno la Kifaransa lenye maana ya Chupa Tupu, imetayarishwa na mkongwe Musa Banzi na itakuwa ikitoa zawadi kwa watazamaji ambao watakuwa wakiangalia na baadae kuja kuulizwa maswali na kujishindia Shilingi elfu hamsini.

Chanzo: Millard Ayo