0

Bingo, Walitesti zali kisha wakanogewa

Bingo, Walitesti zali kisha wakanogewa

Fri, 23 Oct 2020 Source: Mwanaspoti

By KELVIN KAGAMBO KATIKATI ya zaidi ya aina 1000 za muziki duniani kila msanii amechagua kujikita kwenye aina yake ya muziki. Wapo wanaofanya Singeli, K Pop, Jazz, Hip Hop, Blues, Gengetone, Dancehall, Japanoise na mingine huku kila mmoja akiwa na sababu za kuchagua kufanya anachofanya.

Hata hivyo, kwa kawaida wasanii wengi hufanya zaidi ya aina moja ya muziki, lakini bado karibu kila msanii duniani anakuwa na uwanja wake wa nyumbni, aina ya muziki ambayo ndio inayomtambulisha, kwahiyo hata akijaribu kufanya muziki mwingine mwisho wa yote atarudi tu kwenye muziki wake aliozoeleka kuufanya.

Kwa mfano Diamond, anafanya muziki aina ya Afro Pop, huo ndio uwanja wake wa nyumbani, lakini pia mara kadhaa amewahi kujaribu aina nyingine za muziki, amewahi kuimba Mchiriku, Mduara, Zouk, Hip Hop na zaidi lakini mwisho wa yote hurejea kwenye Afro Pop yake.

Lakini pia, kuna wasanii wachache ambao walipata umaarufu kupitia aina fulani ya muziki, lakini baadaye wakajaribu muziki mwingine na walipoona wamepokewa vizuri, wakagoma kurudi kwenye muziki waliokuwa wakiufanya awali — na leo ndo tunawaongelea hao washikaji.

Kumbuka: tunaongelea wasanii ambao walibadilisha aina ya muziki au namna ya uimbaji wakiwa tayari wameshapata ustaa kupitia aina ya muziki au staili ya kuimba waliyokuwa wakiifanya awali.

MBOSSO

Chanzo: Mwanaspoti