0

Bilnass atambia Do Me

Bilnass atambia Do Me

Mon, 9 Nov 2020 Source: HabariLeo

MSANII William Lyimo 'Bilnass' amesema wimbo wake mpya wa ‘Do me’ unaendelea kufanya vizuri kwenye soko la muziki ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesema wakati wimbo huo ukiendelea kushika chati anajipanga kuachia wimbo mwingine kabla mwaka haujaisha.

Bilnass ametoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kuachia wimbo huo aliomshirikisha Faustina Charles ‘Nandy’ ambaye ni mpenzi wake.

Alisema wimbo huo ametoa muda mzuri kwani mashabiki wake kwa kipindi kirefu walikuwa na kiu ya kuona kazi mpya aliyofanya kwa kushirikiana na mwanadada Nandy.

“Wimbo wangu wa Do me unafanya vizuri kwenye soko la muziki ndani na nje ya nchi kwani kwa muda mrefu mashabiki wangu walikuwa na kiu ya kuona kazi mpya niliyomshirikisha msanii Nandy,” alisema Bilnass.

Chanzo: HabariLeo