0

Bele 9 amkubali Young Dee

Bele 9 amkubali Young Dee

Mon, 9 Nov 2020 Source: HabariLeo

MSANII wa Bongo Fleva Abelnego Damian, Bele 9 amesema mwanamuziki David Ganzi, Young Dee, ni miongoni mwa wasanii wanaotazamwa zaidi na wabunifu wa kufanya kazi za kisasa nchini.

Bele 9 aliyasema hayo juzi kwenye uzinduzi wa Albam ya kwanza ya Dee na kusema bado anastahili kuendelea kutazamwa kwani analifahamu vyema soko la kuuzia kazi kwa kuzingatia jamii ya sasa.

“Young Dee ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vitu vipya na mashabiki wanafuatilia kwahiyo anastahili na naheshimu uwezo mkubwa kwake naamini anaenda kupata mafanikio makubwa kutokana na kwamba anafahamu mahitaji ya soko,” alisema.

Alisema kutoa albam yake ya kwanza bado inaendelea kulinda thamani yake kwenye muziki wa bongo fleva nchini ni jambo ambalo wasanii wengi wanashindwa kufanya hivyo kwakuwa kunachangamoto kubwa ya kumuuzia mteja.

Pia Bele 9 amefichua siri ya kupunguza baadhi ya marafiki zake waliokuwa karibu ni kwamba alikuwa anajipanga upya kutimiza malengo aliyojiwekea ya kutafuta watu ambao watakuwa na msaada kwenye kufanya kazi zake za muziki.

“Nimepunguza watu kwasababu lazima niangalie upo kwangu kwasababu gani, ni pointi naipata kwako mpaka niwe karibu na wewe kuna kitu gani tunafanya kama hauna upendo na watu hatuwezi kuwa pamoja, mimi nina malengo ya kufika mbali kwenye shughuli zangu za muziki baada ya kusimama kwa muda mrefu,'' alisema.

Chanzo: HabariLeo