0

Bashungwa: Serikali kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao

E2c28fbf1d83fc20e12ed8c061952c1f Bashungwa: Serikali kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao

Sun, 21 Feb 2021 Source: HabariLeo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila msanii ananufaika na kazi anayofanya kitu kitakachosaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Bashungwa amesema hayo leo jijini Arusha kwenye Kongamano la Fursa kwa Wanamuziki lililoandaliwa na Taasisi ya kijamii inayoshughulika na wanamuziki (TAMUFO) .

“Nimetoa maelekezo kwa Chama cha Haki Miliki (COSOTA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kukamilisha mfumo utakaosidia kutambua kazi za wasanii zinapotumika kwenye redio, televisheni, mabasi na kumbi za starehe” amesema Bashungwa.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuliombea taifa ili Mungu aweze kuliepusha na magonjwa mbalimbali.

Chanzo: HabariLeo