0

20%: TANZANIA HAKUNA WANAMUZIKI BALI KUNA WANARIZIKI

20%: TANZANIA HAKUNA WANAMUZIKI BALI KUNA WANARIZIKI

Fri, 20 Nov 2020 Source: Zanzibar 24

Mkongwe wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Fleva Twety per Cent ameongea kuhusu ujio wake kwenye industry ya Bongo fleva na kuongelea baadhi ya vitu ambayo vinaendelea kwenye tasnia hio.

Twety per Cent ambae alitamba na kujilikana zaidi kwa nyimbo zake, Tamaa mbaya,Yanini malumbano, Naficha, Mama Neema na Nimerudi salama.

Mkongwe huyu ameeleza kuhusu mabadiliko ya muziki wa Bongo Fleva na kueleza kuwa kwa sasa hakuna wana muziki wa wasanii Tanzania bali kuna Wana Riziki.

Aidha ameongeza kusema kuwa walio wengi Tanzania sio wasanii bali wana force kuishi maisha ya kisanii na ndio mana unasikia watu wengi wakihoji juu ya maisha ya msanii flani mfano gari analotembelea badala ya kuhoji kuhusu muziki wake.

“Nashangazwa sana na wasanii wanaoingia studio kila siku kurekodi na hao ndio wanaoharibu muziki kwa sababu wanaharibu misingi wa muziki”

Chanzo: Zanzibar 24