0

Wakamatwa wakisafirisha nyoka na vinyonga

Fri, 12 Mar 2021 Source: millardayo.com

Wizara ya Maliasili na Utalii imewakamata Watanzania wanne wanaotuhumiwa kusafirisha vinyonga hai 74 na nyoka sita kinyume cha sheria na kuwauzia raia wawili wa Czech.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa, vinyonga na nyoka hao walikamatwa Januari 22 mwaka huu nchini Austria na kuhifadhiwa katika hifadhi ndogo ya wanyama nchini humo.

Watuhumiwa hao  wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho, wakikabiliwa  na makosa ya kusafirisha nje wanyamapori hao bila kibali, uhujumu uchumi pamoja na utakatishaji fedha kupitia biashara hiyo.

Dkt. Ndumbaro ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayebainika kufanya biashara ya kusafirisha Wanyamapori hai ndani na nje ya nchi, wakati biashara hiyo imezuiliwa tangu Mei 2016 atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“MIFUPA YANGU IMESAGIKA, MIAKA 13 SIJATEMBEA, SIJIWEZI, NILIKUA NAJIWEZA” – GETRUDE

Chanzo: millardayo.com