0

Wahamaji haramu wakamatwa wakielekea Dar kutafuta kazi

Wahamaji haramu wakamatwa wakielekea Dar kutafuta kazi

Tue, 16 Feb 2021 Source: HabariLeo

Raia sita wa Malawi walioingia nchini bila kibali wamekamatwa Kibaha mkoani Pwani wakiwa safarini kwenda jijini Dar es Salaam kutafuta kazi za kutoa huduma kwenye baa pamoja na shughuli za ususi.

Akidhibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema raia hao wamekamatwa eneo la Tanita mjini Kibaha wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Hiace.

Kamanda huyo amesema kuwa dereva wa gari hilo (jina limehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi) anashikiliwa kwa kosa la kuwasafirisha wahamiaji hao.

Kamanda Nyigesa ametoa onyo kwa madereva na watu wenye tabia ya kusafirisha wahamiaji haramu kuacha mara moja biashara hiyo.

Chanzo: HabariLeo