0

Takukuru yamhoji Mkurugenzi TPA

Takukuru yamhoji Mkurugenzi TPA

Tue, 30 Mar 2021 Source: MTanzania

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya nchini, (TAKUKURU) imemkamata Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari wa Tanzania(TPA), Desudedit Kakoko ili kuhojiwa kuhusu tuhuma za ufisadi.

Kukamatwa kwa, Kakoko kunafuatia kusimamishwa kazi Jumapili iliyopita kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu, ili kupisha uchunguzi kuhusu udokozi wa fedha za umma zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.55.

Rais Samia alimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seri9kali (CAG), Dk. Charles Kichere kuchunguza jinsi Sh bilioni 3.6 zilivyoibiwa kwenye Mamlaka ya bandari.

Ofisa wa Mawasiliano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani, amesema kuwa ni kweli wanamshikilia Mkurugenzi wa Bandari, Kakoko kwenye Makao Makuu ya taasisi hiyo.

Chanzo: MTanzania