0

Shamimu na mumewe wahukumiwa kifungo cha maisha

Thu, 1 Apr 2021 Source: ippmedia.com

Pia Mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali ya Serikali, na dawa walizokutwa nazo kuteketezwa.

Pia Mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali ya Serikali, na dawa walizokutwa nazo kuteketezwa. Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa Leo Machi 31, 2021 na Jaji Elinaza Luvanda, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba watuhumiwa wamekutwa na hatia kwa makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, walikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 439.70, na walidaiwa kutenda tukio hilo Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Chanzo: ippmedia.com