0

Mwalimu adakwa kwa kujiunganishia maji kinyemela  

Sat, 13 Mar 2021 Source: www.habarileo.co.tz

MWALIMU mmoja anayefundisha katika shule ya sekondari Makongoro iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara, anatuhumiwa kujiunganishia isivyo halali mtandao wa maji ya bomba na kuisababishia hasara Mamlaka ya Maji ya Mji wa Bunda (BUWSSA).

alibainisha hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa kikosi kazi cha mamlaka hiyo kiligundua hujuma hiyo wakati wa ukaguzi wa miuondombinu ya maji.

Alisema kuwa baada ya kikosi kazi hicho kufika nyumbani kwa mwalimu huyo katika mtaa wa Idara ya maji, kata ya Bunda Stoo mjini Bunda, ndipo wakakuta amejiunganishia mtandao wa maji kwa njia isiyo halali.

Kaimu Ofisa mahusiano wa BUWSSA, Daniel Ngeleja, alisema kwamba kutokana na hujuma kama hiyo wamekuwa wakipata hasara ya upotevu wa maji kwa zaidi ya asilimia 32.

Diwani wa kata ya Bunda Stoo Joseph Nyamageko na Ofisa Mtendaji wa mtaa wa Idara ya Maji, Witness Kuleba pamoja na wananchi wa kata hiyo ambao siku hiyo walikuwa katika eneo la tukio hilo, wote kwa pamoja wamesikitishwa na kitendo hicho, wakisema kuwa kuhujumu miundombinu ya maji kunasababisha wananchi wengine kukosa huduma hiyo ya maji na kisha kuanza kuilalamikia serikali.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baada ya kupata dhamana ya polisi, mwalimu huyo alikanusha kujiunganishia mtandao wa maji na kusema kuwa hiyo ni chuki binafisi ya watu wa BUWSSA.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa BUWSSA, Maisha alitoa wito kwa wananchi kuacha kuhujumu miuondombinu ya miradi ya maji, kwani yoyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria, ambapo atapigwa faini au kupewa adhabu ya kifungo ama vyote viwili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz