0

MGONJWA AMUUA MUUGUZI KWA KUMCHOMA KISU

Mon, 8 Mar 2021 Source: zanzibar24.co.tz

Agatha Mbalalila (50) amefariki baada ya mmoja ya Wagonjwa kudaiwa kumchoma kisu wakati akielekea kuwahudumia Wagonjwa wengine huko katika kituo Mtawa Muuguzi wa Kituo cha kuhudumia Wagonjwa wa Ukoma cha Nazareth kilichopo Ifakara,

Kakizungumzia tukio hilo katibu wa Kituo cha Nazareth, Ladislaus Mloti amesema marehemu alimpokea mtuhumiwa Februari 27, 2021 baada ya kufika kituoni na kujieleza kuwa ametoka katika matibabu ya Ukoma Wilaya ya Bagamoyo

Amesema mtuhumiwa hakuwa na matatizo ya akili wakati anapokelewa na waliamua kumlaza ili kumpatia matibabu ya vidonda alivyokuwa navyo mguuni na baada ya kupona wangemruhusu arudi nyumbani.

Chanzo: zanzibar24.co.tz