0

Wataka soko ili walipe kodi

Wataka soko ili walipe kodi

Tue, 3 Nov 2020 Source: HabariLeo

Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Kamanga jijini Mwanza wameiomba serikali kuwajengea eneo rasmi la kufanyia biashara ili waweze kuongeza wigo wa shughuli zao.

Mwenyekiti Msaidizi wa Soko, Raphael Magambo, amesema sio tu kuongeza wigo bali wanahitaji kuanza kulipa kodi kwani wameshakomaa kibiashara na kuvuka hatua ya umachinga.

“Soko hili ni finyu na mazingira ya kibiashara kwa ujumla sio rafiki kama unavyoona wengine wanafanyia shughuli zao barabarani. Tulianza wafanyabiashara wapatao 20 na sasa ni zaidi ya 500, kwahiyo unaweza kuona ni kiasi gani hapa hapatufai tena, tuonaomba kujengewa soko rasmi katika mwambao huu huu wa Ziwa,” amesema.

Chanzo: HabariLeo