0

Wafanyabiashara pangeni bidhaa maeneo safi

Tue, 6 Apr 2021 Source: ippmedia.com

Yuna aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi habari baada ya uchaguzi wa viongozi wa wafanyabiashara wa soko la sabasaba, jijini humo.

Afisa huyo alisema kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo kwa wafanyabiashara wakahakikisha maeneo wanayofanyia biashara yanazingatia afya za walaji na kikidhi soko la ushindani wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.

“Rai yangu hapa ninawaomba wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira yenye ubora na kuzingatia kanuni za kiafya,hii itawafanya kuwavutia wateja na walaji wa bidhaa zao,na pia itawafanya kuingia kwenye ushindani wa biashara,”alisema.

Aliwasisitiza kuheshimu na kutii kanuni na taratibu katika ufanyaji biashara na kujiepusha kuvamia maeneo yasiyo rafiki ambayo hayaruhusiwi.

Alisema pamoja na uhuru walionao wa kufanya biashara wafanyabiashara wanawajibu wa kushirikiana na Jiji katika kuhakikisha maeneo yasiyo rasmi wanayaepuka na kufuata maelekezo yanayotolewa.

Kuhusu viongozi wa soko la sabasaba, Ofisa huyo aliwaomba kuhakikisha wanashirikiana na Jiji ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni na maelekezo yanayotolewa.

Chanzo: ippmedia.com