0

Uhondo wa Usiku wa Ulaya umerejea kupitia DStv

Uhondo wa Usiku wa Ulaya umerejea kupitia DStv

Tue, 20 Oct 2020 Source: Mwanaspoti

Uhondo wa Usiku wa Ulaya umerejea kupitia DStv

Ule usiku wa Ulaya uliokua unasubiriwa kwa hamu kwelikweli na mashabiki wa soka dunia nzima umerudi tena. Ligi ya mabingwa Ulaya imerudi tena kwa moto wa hali ya juu kwa ufunguzi wa mechi kali na tamu zitakazopigwa Jumanne na Jumatano wiki hii.

Ligi hiyo ambayo inahusisha vilabu bingwa kutoka kwenye mataifa ya Ulaya inafungua pazia la msimu wa mwaka 2020/21 kwa mitanange mbalimbali ya hatua ya makundi.

Viwanja takribani 16 vitatumika kuamua matokeo muhimu sana. Mechi zitapigwa kuanzia Saa 20:00 na zingine saa 22:00 usiku wa Jumanne na Jumatano.

Moja kati ya mitanange inayaosubiriwa kwa hamu katika wiki ya kwanza ya ufunguzi wa pazia la michuano hii ni mechi kati ya PSG watakao waalika Man United siku ya Jumanne na bingwa mtetezi Bayern Munich ataanza safari ya kutetea taji hilo kwa kuwakaribisha vijana wagumu wa Diego Simeone, Atletico Madrid siku ya Jumatano.

Ukiachana na mechi hizo kali lakini pia kwa wapenzi wa timu za Uingereza wana hamu ya kuona vilabu vyao vitaanzaje msimu huu mpya wa mwaka 2020/2021. Baadhi ya timu za Uingereza zitakazoanza kampeni zao wiki hii ni; Chelsea vs Sevilla, Man city vs Porto na Ajax vs Liverpool.

Chanzo: Mwanaspoti