0

Serikali kutoa umeme wa kutosha

Serikali kutoa umeme wa kutosha

Wed, 18 Nov 2020 Source: HabariLeo

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha hapa nchini ambao utapatikana kwa gharama nafuu.

Majaliwa amesema hayo hii leo mkoani Pwani kwenye uzinduzi wa njia ya mchepuko kupitisha maji kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere .

Amesema kuwa serikali itaipa kipaumbele sekta ya nishati ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa umeme inaimarika kama njia mojawapo ya kusogeza huduma za kijamii na maendeleo kuwafikia wananchi.

Amesema upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa bei nafuu utachochea ukuaji wa sekta ya viwanda kwa kushusha gharama za uendeshaji jambo litakalosaidia kukabiliana na mfumuko wa bei.

Chanzo: HabariLeo