0

Safari za ndege zaanza kurejea kawaida

Tue, 13 Oct 2020 Source: habarileo.co.tz

TANZANIA imefungua anga na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, huku mashirika mbalimbali ya ndege yakianza kuingia na kutoka nchini.

Hatua hiyo inatokana na maambukizi ya virusi vya corona kuanza kupungua katika nchi hizo, huku taratibu za kujikinga zikiimarishwa katika viwanja vya ndege.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, akizungumza na HabariLEO juzi, alisema mamalaka hiyo imeshafanya kazi yake ya kuhakikisha anga linafunguka hivyo ndege zinaweza kufanya safari kuingia na kutoka nje ya Tanzania.

“Mamlaka imetimiza lengo lake la kuhakikisha anga linafunguka na tayari kwa nchi zote za Afrika Mashariki anga liko tayari kwa safari baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona,” alisema.

Alisema mwingiliano wa usafiri wa anga katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Sudan Kusini, Rwanda na Tanzania sasa inawekana na kwamba baadhi ya mashirika ya ndege yameanza safari wakati kampuni nyingine zikijiandaa kurejea kwa kuzingatia hali ya biashara.

Alisema shirika la ndege la Uganda limeishaanza kufanya safari za kuingia nchini, huku Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) likiendelea kujipanga kuanza safari kwenda Entebbe hivi karibuni.

Taarifa ya shirika la ndege la Uganda lilieleza hivi karibuni kurejesha safari zake nchini baada ya kusitishwa kuanzia Machi kutokana na kulipuka kwa virusi wa corona

Shirika hilo lilisema kutakuwa na safari mara nne kwa wiki katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili kwenda jijini Dar es Salaam

huku wakitarajia kuongeza safari katika miezi ijayo.

Mkurugenzi wa biashara wa shirika hilo, Roger Wamala alisema licha ya kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo wamedhamiria kuendelea na safari za Tanzania .

Wamala aliongeza kuwa shirika hilo limedhamilia usalama na afya kwa kufata za kukabiliana na ugonjwa huo kitaifa na kimataia ikiwemo kuzingatia umbali wa kukaa kwa abiria,kuvaa barakoa ,kupima joto na kutumia vitakasa mikono.

Johari alisema kwa ndege za Kenya,tayari hivi karibuni ,Shirika la ndege la nchi hiyo zimeanza zake kuelekea Kilimanjaro mara tatu kwa wiki na safari za Zanzibar zikitarajiwa mara mbili kwa wiki.

Alisema ndege za nchini ikiwemo precision Air imeishaanza safari zake juzi kuelekea nchini humo kama ilivyokuwa awali.

Ofisa mtendaji mkuu wa Kenyairways ,Alln Kilavuka alisema wameanza safari zake kwenda Dar es Salaam na Zanzibar , Tanzania ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Kenya na Afrika Mashariki na tunatarajia ushirikiano wetu kuendelea.

Ndege ya kwanza ya Kenya Airways kwenda Dar es Salaam iliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta - Nairobi asubuhi ya Jumatatu Septemba 21 na ya pili jioni ya 3 Septemba 23 mwaka huu Baada ya hapo KQ itafanya safari mbili za kila siku kwenda Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa KQ kwenda Zanzibar ilianza safari Septemba 26 na baadaye kuendelea na safari zake mara tatu kwa wiki - Jumatatu, Jumatano na Jumamosi huku Ndege za kwenda uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro zikianza mwezi huu ili kulenga kuunganishwa na njia ya Nairobi- New York.

Alisema kwa nchini Rwanda,Tayari shirika la ndege la nchi hiyo la Rwandair limeanza kufanya safari zake nchini ,lakini kwa ATCL hata kabla ya kulipuka kwa ugonjwa huo hakukuwa na safari za Rwanda hivyo usafiri unafanyika kama kawaida na anga lake limeishafunguliwa.

Johari alisema nchini Rwanda kuna ndege ndogo toka Tanzania ndiyo zilikuwa zikifanya safari zake nchini him,o na zinaendelea kulingana na mahitaji ya kibiashara.

Alisema pia anga la nchi ya Sudani kusini nalo limefunguliwa na mashirika ya ndege yataendelea kufanya safari kulingana na mahitaji ya kibiashara.

Chanzo: habarileo.co.tz