0

Rais Magufuli azuia tozo wenye vitambulisho

Rais Magufuli azuia tozo wenye vitambulisho

Thu, 22 Oct 2020 Source: HabariLeo

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli amesema atahakikisha wananchi wa Jimbo la Hai hawalipi tozo yoyote ya mazao kwa mzigo usiozidi tani moja kwa mtu yoyote atakayekuwa na Kitambulisho cha Ujasiriamali ambacho kwa mwaka kinagharimu Tsh. Elfu 20.

Dk. Magufuli amebainisha hayo alipokuwa katika mwendelezo wa kampeni zake jimboni humo na kuongeza ili kufanikisha hayo kwa miaka mitano ijayo wananchi wanapaswa kumchagulia wabunge na madiwani kutoka chama hicho.

Aidha, Dk. Magufuli amesema kuwa iwapo atapata ridhaa ya wananchi kuongoza tena atahakikisha ujenzi wa soko la kisasa la mazao katika eneo la Sadala unakamilika mara moja.

Chanzo: HabariLeo