0

RC Tanga "Nitawashughulikia wote wanaouza Cement bei juu" (+video)

Video Archive
Wed, 11 Nov 2020 Source: Millard Ayo

November 11, 2020 Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wa Cement kwa yeyote atakaepandisha bei.

Hayo ameyazungumza baada ya kutembelea viwanda vya Simba cement pamoja na Kilimanjaro cement kutaka kujua hali ya uzalishwaji wa bidhaa hiyo pamoja na bei za cement zinazouzwa viwandani hapo.

Shigella amesema kuwa amefarijika sana kwa sababu bei ya uzalishaji na bei ambayo inauzwa hapo  viwandani bado haijabdilika  hivyo matarajio yao kwa wafanya biashara, wanunuzi pamoja na wasafirishaji ni kutokupandisha bei inatakiwa ibaki ileile iliyokuwa ikiuzwa katika kipindi cha miezi mitatu nyuma iliyopita.

” Kwa hiyo nikiona au kusikia Kuna cement inapandishwa bei katika jiji letu la Tanga basi huyo mfanya biashara ajiandae kufanya biashara nyingine au atafute sehemu nyingine ya kufanyia biashara” Shigella.

“Na yeyote atakae kuwa anakwenda kinyume maafisa biashara chukueni hatua ikiwa ni pamoja na kuwanyima leseni ili waweze kufanya shughuli nyingine ambazo wanataka kuzifanya “ Shigella.

Chanzo: Millard Ayo