0

Pwani watoa bil 2.1/- mikopo ya asilimia 10

Pwani watoa bil 2.1/- mikopo ya asilimia 10

Sun, 4 Apr 2021 Source: HabariLeo

MKOA wa Pwani katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 umetoa Sh bilioni 2.1 ambazo ni asilimia 10 za mapato ya halmashauri tisa za mkoa huo ambapo hadi kufikia Februari mwaka huu fedha marejesho zilizokusanywa ni Sh bilioni 1.7 sawa na asilimia 78.5 ya fedha zilizopangwa kutolewa katika kipindi hicho.

Hayo yalisema mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo wakati wa makabidhiano ya utoaji wa mikopo ya fedha taslimu na vifaa kwa wajasiriamali kupitia (Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019) na ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025.

Ndikilo alisema kuwa fedha ambazo zimetolewa kwenye vikundi hadi Februari 2021 ni Sh bilioni 1.1 sawa na asilimia 66.9 ambapo hali ya utoaji mikopo hiyo na marejesho mkoani hapo mwaka 2019/2020 jumla ya shilingi zilitolewa ni Sh bilioni 2.6.

“Mwaka jana fedha hizo zilitolewa kwa vikundi 672 sawa na asilimia 108 ya fedha zilizopangwa kutolewa na marejesho yalikuwa Sh milioni 645.7 sawa na asilimia 54 ya fedha zilizokopeshwa kwa kipindi hicho kupitia silimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hizo kwenye mkoa wetu,” alisema Ndikilo.

Akikabidhi fedha na vifaa vyenye thamani ya shilingi 245.8 kupitia mikopo ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya Mji Kibaha kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye walemavu fedha ni Sh milioni 177.7 na vifaa vilivyokabidhiwa ni pikipiki 12, bajaji moja, toyo moja na mashine moja ya kutengenezea sabuni kwa vikundi 68 vya wajasiriamali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Jenifa Omolo alisema kuwa moja ya mafanikio waliyopata ni pamoja na kujenga kituo cha biashara katika soko la Mnarani maarufu kama Loliondo ambacho wajasiriamali wanapata sehemu ya kuuza bidhaa zao wakiwa kwenye eneo moja.

Omolo aliwataka wanawake wajasiriamali kutumia jengo la wajasiriamali lililojengwa katika soko la Mnarani ambalo limejengwa na Halmashauri hiyo lakini halitumiki kama ilivyopangwa na moja ya vikwazo wanavyokumbana navyo kwenye utoaji wa mikopo ni pamoja na kundi la vijana na watu wenye ulemavu kutotumia vizuri mikopo hali inayosababisha marejesho kuchelewa.

Chanzo: HabariLeo