0

Nyasaka kujengwa masoko mawili

Wed, 7 Oct 2020 Source: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Nyasaka kuwajenga masoko mawili katika kata hiyo.

Mabula alisema hayo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Nyasaka center,Dk Mabula alisema Watajenga soko katika eneo la Nyasaka center na Nyambuge.

Alisema Katika kipindi cha miaka mitano nikiwa kama mbunge kwa kushirikiana na wananchi waliokuwa wakianzisha misingi na ofisi ya mbunge alitoa tofari zote na halmashauri ya manispaa ya Ilemela kuezeka na wakafanikiwa kuanzisha shule mpya za msingi 4 ambazo ni Ihalalo, Bezi na Kayenze ndogo pamoja na Shule ya Msingi Kisundi na kufanya shule za msingi kuongezeka kutoka 72 mwaka 2015 mpaka shule 76 mwaka 2020.

Alisema katika shule ya msingi ya Nyasaka wamefanikiwa kutoa matofali 1500,saruji mifuko 50, madawati 80 na wamejenga madarasa matatu yenye thamani ya shilingi milioni 68/-.

Dk Mabula aliwaahidi wakazi wa kata hiyo,kuwa atawajengea barabara za rami kuanzia eneo la Nyambuge-Nyambiti,Airport-Nyanguge.

Alisema katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020, kwa kushirikiana na wananchi pamoja na halmashauri nimefanikiwa kuanzisha shule mpya tatu ambazo ni Kayenze, Angeline Mabula na Kisundi za kidato cha kwanza hadi cha nne nakufanya Halmashauri kuwa na sekondari 27 za Serikali. Jumla ya wanafunzi 27,811 wamesajiliwa katika Shule za Sekondari za Serikali.

Chanzo: habarileo.co.tz